• HABARI MPYA

    Saturday, December 28, 2013

    TAZAMA MAYWEATHER 'ALIVYOWATANDIKA' PACQUIAO, AMIR KHAN NA MAIADANA

    BONDIA Floyd Mayweather amefufua vita ya maneno na mpinzani wake, Manny Pacquiao pamoja na kuwakandia pia Amir Khan na Marcos Maidana kwa staili ile ile.
    Pamoja na kumuita Pacquiao majeruhi wa Juan (Manuel) Marquez akikumbushia kipigo cha Mfilipino huyo mwishoni mwa mwaka 2012 kwa Knockout (KO) kutoka kwa Mmexico huyo, Mayweather ameweka picha ya 'kubumba' akiwa amemsukumia konde zito usoni.
    "Sasa unaniambia nakwenda kula makombo ya Juan Marquez? Acha nizungumze na IRS juu ya hili," alitweet mbabe huyo.
    Hizi ni salamu: Floyd Mayweather (kushoto) akimsukumia konde Manny Pacquiao, kuashiria pambano baina yao linaweza kuokea

    Awali iliripotiwa, Khan anajiandaa kuwa mpinzani ajaye wa Mayweather mwezi Mei, lakini Mmarekani huyo ameendelea kuwaambia mashabiki wake kwamba ataendeleza ubabe wake.
    Kama ambayo wengi wanchukulia Khan atakuwa mpinzani dhaifu kwa Mayweather, bondia huyo naye amembeza akimuita 'Con Artist' katika picha ambayo amebandika ya kubumba akimchapa konde hadi kuelekea sakafuni. Amesema: "Hebu fikiria, nini Amir "Con Artist" atapata kama atachaguliwa kuingia anga za Mayweather,".
    Mtu mwingine anayechukuliwa kama mpinzani wa baadaye wa bondia huyo bingwa wa madaraja matano ya uzito duniani ambaye hajawahi kupigwa ni Muargentina, Maidana, kufuatia ushindi wake wa kushitua dhidi ya mbabe aliyepewa jina 'New Mayweather', Adrien Broner.
    Akiwa amebandika picha kama hizo,akimtandika ngumi ya mkono wa kulia, Mayweather pia ametweet kuhusu bondia huyo: "Naweza kuagiza kipande kimoja na biskuti tafadhali? Hakuna sehemu."
    Floored: Floyd Mayweather appears most likely to meet Britain's Amir Khan next, in May
    Sakafuni: Floyd Mayweather ameweka picha akimuadhibu Muingereza Amir Khan, pambano lao linatarajiwa kufanyika Mei
    Power puncher: But Floyd Mayweather would clearly be confident of beating Marcos Maidana (left)
    Konde la nguvu: Lakini Floyd Mayweather anajiamini pia atampiga Marcos Maidana (kushoto)
    Pound-for-pound king: Floyd Mayweather has long been considered the best fighter in the world
    Mfalme wa masumbwi: Floyd Mayweather amekuwa akipewa heshima ya bondia bora kwa muda mrefu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAZAMA MAYWEATHER 'ALIVYOWATANDIKA' PACQUIAO, AMIR KHAN NA MAIADANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top