• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 17, 2013

  SUAREZ ABEBA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA

  MSHAMBULIAJI Luis Suarez ametajwa mchezaji bora wa mwaka wa tuzo ya Shirikisho la Mashabiki wa Soka jana usiku.
  Kiasi kisichozidi miezi sita baada Arsenal kutaka kumnunua kwa Pauni 40,000,001 nyota huyo wa Uruguay, Suarez aliinua tuzo hiyo Emirates.
  Lakini ilikuwa ni tuzo binafsi kwa mshambuliaji huyo wa anayemtoa udenda kocha Arsene Wenger, akiwapiku Leighton Baines, Christian Benteke, Juan Mata, Robin van Persie na Pablo Zabaleta kushinda tuzo hiyo iliyohusisha wapiga kura zaidi ya 500,000.
  Mshindi: Mchezaji Bora wa Mwaka, Luis Suarez akisherehekea tuzo yake ya Shirikisho ya Mashabiki wa Soka, akiwa na mkewe Sofia
  Mshambuliaji huyo wa Liverpool, aliyehudhuria shughuli hiyo Emirates, alisema: "Nafikiri ni haki kusema mwaka uliopita ulikuwa mzuri kwangu. 
  "Tuzo hii si yangu peke yangu, ni pamoja na wachezaji wenzangu, uongozi na benchi la Ufundi na yeyote anayehusiana na Liverpool,". 
  Eventful year: Suarez celebrates with his award at the Emirates Stadium
  Suarez akisherehekea na tuzo yake Uwanja wa Emirates
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUAREZ ABEBA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top