• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 14, 2013

  CHELSEA YAKARIBIA KUIENGUA ARSENAL KILELENI ENGLAND

  MABAO ya Fernando Torres dakika ya 16 na Ramires dakika ya 35 yameipa ushindi wa 2-1 Chelsea dhidi ya Crystal Palace jioni ya leo Uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Bao pekee la Crystal lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Chamakh dakika ya 29. 
  Ushindi huo unamaanisha Chelsea inaweza kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England ikiifunga Arsenal Desemba 23 Uwanja wa Emirates.  
  Katika mechi nyingine za Ligi hiyo leo, Manchester City imeifunga 6-3 Arsenal, Cardiff City imeilaza 1-0 West Bromwich, Everton imeikung'uta 4-1 Fulham, Newcastle United imetoka 1-1 na Southampton, West Ham United imetoka 0-0 na Sunderland sawa na Hull City na Stoke City.

  La ushindi: Ramires ameifungia Chelsea bao la pili leo kuipa pointi tatu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAKARIBIA KUIENGUA ARSENAL KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top