• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 26, 2013

  MAN UNITED YATAKA KUVUNJA REKODI YA DAU LA USAJILI KWA KUMSAINI KIUNGO HATARI WA DURTMUND

  KLABU ya Manchester United imeonywa kwamba mchezaji chaguo la kwanza la David Moyes katika usajili wa dirisha dogo, Marco Reus atawagharimu hadi Pauni Milioni 40 ili kumpata. 
  Kiungo Reus ana thamani ya Pauni Milioni 29.4 Borussia Dortmund.
  Lakini inafahamika mambo yamebadilika tangu Bayern Munich ionyeshe nia ya kutaka kumsajili Mario Gotze.
  Itakugharimu! Borussia Dortmund inataka dau la Pauni Milioni 40 ili kumuuza Marco Reus, ambaye anatakiwa na Manchester United katika usajili wa Januari
  World class: United would have to break their transfer record to sign the talented Reus, whom manager David Moyes has identified as a key target to galvanise their midfield
  Kiwango cha dunia: United itavunja rekodi ya dau la usajili kumsajili mchezaji mwenye kipaji, Reus, ambaye kocha David Moyes amemtambulisha kama chaguo la kwanza katika wachezaji anaowataka

  Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England watatakiwa kuvunja rekodi yao ya dau la usajili ili kuipata saini ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.
  Wasaka vipaji wa United wakuwa wakisaka mchezaji wa kiwango cha dunia kwa nafasi yoyote. 
  Pamoja na hayo, kiungo huyo anabakia kuwa chaguo lao la kwanza, ingawa pia wanasaka na washambuliaji, beki wa kushoto na beki wa kati waje kuwa warithi wa Patrice Evra na Rio Ferdinand mwishoni mwa msimu.
  Nearing the end? United have started the search for Patrice Evra's replacement
  Anaelekea mwisho? United imeanza kusaka mbadala wa Patrice Evra
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATAKA KUVUNJA REKODI YA DAU LA USAJILI KWA KUMSAINI KIUNGO HATARI WA DURTMUND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top