• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 21, 2013

  MAN CITY MOTO BATI ENGLAND, SASA YA TATU

  MSHAMBULIAJI Jesus Navas aliyetokea benchi na James Milner walimfutia makosa beki Vincent Kompany kwa kufunga mabao yaliyoipa Manchester City ushindi wa 4-2 dhidi ya Fulham Uwanja wa Craven Cottage.
  Baada ya Kompany kujifunga zikiwa zimesalia dakika 20 na kufanya timu hizo ziwe zimefungana 2-2, Navas na Milner wakaibeba City kwa mabao yaliyoipandisha timu hiyo nafas ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
  Wiki moja baada ya kuifunga Arsenal 6-3 nyumbani, mabao ya City yalifungwa na Toure dakika ya 23, Kompany dakika ya 43, Navas dakika ya 78 na Milner dakika ya 83, wakati ya wapinzani moja alifunga Richardson dakika ya 50 na lingine Kompany akajifunga dakika ya 69.
  Mkombozi: Jesus Navas amefunga bao dakika za mwishoni kuipa ushindi Manchester City dhi ya Fulham Uwanja wa Craven Cottage
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY MOTO BATI ENGLAND, SASA YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top