• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 14, 2013

  YANGA YAICHAPA KMKM 3-2 KASEJA LANGONI

  Na Saada Akida, Dar es Salaam
  YANGA SC imeifunga KMKM ya Zanzibar mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Jerry Tegete akimalizia pasi ya kichwa ya Mrundi, Didier Kavumbangu.
  Kipindi cha pili, Yanga SC ilirejea na moto wake na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akaipatia bao la pili dakika ya tatu tu tangu kuanza kipindi hicho, dakika ya 48 akiunganisha kwa kichwa mpira wa kurushwa wa beki mwenzake, Mbuyu Twite.
  Kikosi cha Yanga SC kilichoifunga KMKM 3-2 leo

  KMKM walifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 69 lililofungwa na Hajji Simba aliyeingia kuchukua nafasi ya Ame Khamis. Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Ally Ahmed ‘Shiboli’ aliisawazishia KMKM dakika ya 72 akiunganisha krosi nzuri ya Juma Mbwana.
  Kiungo Khamis Thabit aliifungia Yanga SC bao la ushindi dakika ya 78 kwa shuti kali akiwa ndani ya eneo la hatari. Kocha mpya wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic alikuwepo uwanjani kuwaangalia Yanga wanavyocheza kwa kuwa atamenyana nao wiki ijayo katika mchezo wa Nani Mtani Jembe unaoandaliwa na wadhamini wa timu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA KMKM 3-2 KASEJA LANGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top