• HABARI MPYA

    Monday, December 23, 2013

    SIMBA NA YANGA MTANI JEMBE YAINGIZA MILIONI 400 NA UPUUZI

    Na Prince Akbar, Ilala
    MECHI ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema kwamba mapato hayo ni kutokana na mashabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
    Mashabiki wa Simba SC siku hiyo

    Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.
    Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA MTANI JEMBE YAINGIZA MILIONI 400 NA UPUUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top