• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 21, 2013

  AZAM, SHOOTING TIKETI ZA ELEKTRONIKI

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya matumizi ya tiketi za elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
  Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniphace Wambura amesema kwamba mechi ya kwanza itakuwa Desemba 26 mwaka huu saa 10 jioni ambapo itazikutanisha timu za Azam na Ruvu Shooting. Mechi nyingine itachezwa Januari Mosi mwakani kwa kuzikutanisha Ashanti United na JKT Ruvu.
  Azam FC

  Amesema TFF inatoa wito kwa mashabiki kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali ya kushuhudia burudani pia watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za elektroniki unavyofanya kazi.
  Amesema kwa kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya tiketi za elektroniki, TFF imepanga vilevile kuandaa mechi nyingine majaribio mikoani kabla ya mfumo huanza kutumika rasmi Januari  25 mwakani katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM, SHOOTING TIKETI ZA ELEKTRONIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top