• HABARI MPYA

    Tuesday, December 10, 2013

    MANJI ABWAGA MANYANGA YANGA, AWATEUA SEIF MAGARI NA BENNO VILLA KUWA VIONGOZI WAPYA JANGWANI

    Na Mwandishi Wetu, Jangwani
    MWENYEKITI wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Yussuf Mehboob Manji amesema hatagombea tena nafasi hiyo baada ya kumaliza muda wake Julai mwakani.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam, Manji amesema ameamua mwenyewe kutogombea bila shinikizo na kikubwa amefuata demokrasia.
    Manji kushoto, akizungumza na Waandishi wa Habari leo na kulia ni Beno Njovu katikati, Ofisa Habari wa klabu, Baraka Kizuguto 
    “Nina miezi saba kabla ya uchanguzi mkuu mwakani, hivyo sasa ninajitahidi kukamlisha shughuli zote ambazo nilianza kuzifanya ndani ya Yanga nikiwa kama Mwenyekiti ili uongozi mpya utakaoingia uweze kuendeleza mipango ya kuifanya Yanga iwe klabu bora Tanzania,”alisema.
    Pamoja na hayo, Manji amemtambulisha Beno Njovu kuwa Katibu Mkuu mpya wa klabu, akichukua nafasi ya Lawrence Mwalusako aliyekua anakaimu kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.
    Manji amesema Beno Njovu anaanza kuitumikia hiyo nafasi mpya kuanzia leo na Mwalusako atakua naye pamoja kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi atakapomkabidhi kazi rasmi.
    Aidha, Manji amesema Mkutano Mkuu wa wanachama utafanyika Januari 19, mwakani na wanachama watapata fursa ya kupitia taarifa ya mapato na matumizi pamoja kujadili ajenda nyingine mbalimbali.
    Pamoja na hayo, Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki, kimemteua Seif Ahmed ‘Magari’ kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa na kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Utendaji. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI ABWAGA MANYANGA YANGA, AWATEUA SEIF MAGARI NA BENNO VILLA KUWA VIONGOZI WAPYA JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top