• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 28, 2013

  DZEKO AIPAISHA KILELENI MAN CITY LIGI KUU ENGALND, WELBECK NAYE AITAKATISHA MAN UNITED UGENINI

  BAO la dakika ya 66 la Edin Dzeko limeipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England jioni hii.
  Hilo ni bao la 50 kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Bosnia tangu ajiunge na Manchester City, ambalo linaipa timu yake ushindi wa 10 mfululizo Uwanja wa nyumbani, Etihad.
  Man City sasa imetimiza pointi 41, baada ya kucheza mechi 19 na kusimama kileleni mwa Ligi Kuu England, ikiipiku Arsenal inayobaki na pointi zake 39, ingawa imecheza mechi 18.  
  Kiulaini anatumbukiza: Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko akimtungua kipa Julian Speroni kuipa timu yake ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace
  Man of the moment: Dzeko (right) celebrates his goal as Palace's players look on in frustration after conceding
  Dzeko (kulia) akishangilia baada ya kufunga
  Relief: Dzeko is congratulated by Alvaro Negredo (left) after breaking the deadlock at the Etihad Stadium
  Dzeko akipongezwa na wenzake, Alvaro Negredo (kushoto) baada ya kufunga bao pekee Uwanja wa Etihad

  Katika mchezo mwingine, bao pekee la Danny Welbeck dakika ya 57 limeipa Manchester United ushindi wa 1-0 pia dhidi ya Norwich ugenini.
  Ushindi huo, unaifanya United ifikishe pointi 34 baada ya kucheza mechi 19 na kubaki nafasi ya sita, nyuma ya Everton yenye poinyi 36 pia, Liverpool pointi 36 na Chelsea 37.  
  Goal! Danny Welbeck scored soon after coming on to win the game for Manchester United
  Shujaa! Danny Welbeck akishangilia bao lake pekee aliloifungia Manchester United leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DZEKO AIPAISHA KILELENI MAN CITY LIGI KUU ENGALND, WELBECK NAYE AITAKATISHA MAN UNITED UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top