• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 28, 2013

  NEYMAR NOUMAAAA, APIGA TANO PEKE YAKE MECHI LA HISANI LA MASTAA BRAZIL

  WAKATI La Liga ikiwa mapumzikoni, nyota wa Barcelona, Neymar alitumia nafasi hiyo kurejea Brazil kushiriki mchezo maalum wa hisani dhidi ya mchezaji wa zamani wa Paris Saint-Germain na AC Milan, Leonardo.

  Marafiki wa Neymar waliwafunga Marafiki wa Leonardo mabao8-6 huku Neymar akifunga mabao matano na kuonyesha uwezo mkubwa sana wa kandanda pamoja na kuonyesha tattoo yake mpya.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atarejea Hispania mapema Januari akidhamiria kuiongoza Barca katika mashindano ya nyumbani na Ulaya kwa mafanikio, kabla ya kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia nyumbani kwao, Julai mwakani.


  Kitu kipya: Neymar ameonyesha tattoo yake mpya wakati wa mechi ya hisani mjini Goiania, Brazil
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NEYMAR NOUMAAAA, APIGA TANO PEKE YAKE MECHI LA HISANI LA MASTAA BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top