LONDON, England
MABAO ya Nicklas Bendtner dakika ya pili na Mesut Ozil dakika ya 47 yameipa ushindi wa 2-0- Arsenal dhidi ya Hull City jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana.
Mabingwa watetezi Manchester United, wamezamishwa nyumbani na Everton bao pekee la Bryan Oviedo.
Luis Suarez amefunga mabao manne katika ushindi wa 5-1 wa Liverpool dhidi ya Norwich, wakati bao lingine limefungwa na Raheem Sterling, huku bao la wapinzani likifungwa na Johnson.
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 wa Manchester City dhidi ya West Brom, bao lingine likifungwa na Aguero huku mabao ya wapinzani yakifungwa na Pantilimon na Anichebe.
Chelsea ilipata ushindi wa mbinde wa 4-3 ugenini dhidi ya Sunderland, mabao yake yakifungwa na Frank Lampard, Hazard mawili na Bardsley aliyejifunga, wakati mabao ya wenyeji yalifungwa na Altidore na Bardsley.
Fulham walitangulia kupata bao kupitia kwa Dejagah kipindi cha pili, lakini Chiriches akaisawazishia Tottenham Hotspur na Holtby akaifungia la ushindi.
Everton wakishangilia jana
Mana City wakishangilia jana
Baada ya matokeo ya mechi za jana usiku, Arsenal inaendelea kuongoa Ligi Kuu England kwa pointi zake 34 ilizovuna kwenye mechi 14, Chelsea ya pili kwa pointi zake 30 mechi 14 pia, Man City ya tatu pointi 28 mechi 14 pia, Liverpool ya nne pointi 27 mechi 14 pia Everton ya tano pointi 27 mechi 14 pia na Spurs ya sita pointi 24 mechi pia, wakati mabingwa watetezi, United wenye pointi 22 wapo nafasi ya tisa.

![]() |
| Bendtner akishangilia bao lake jana na chini ni Luis Suarez aliyeifungia manne Liverpool akishereheka kazi yake jana |
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 wa Manchester City dhidi ya West Brom, bao lingine likifungwa na Aguero huku mabao ya wapinzani yakifungwa na Pantilimon na Anichebe.
Chelsea ilipata ushindi wa mbinde wa 4-3 ugenini dhidi ya Sunderland, mabao yake yakifungwa na Frank Lampard, Hazard mawili na Bardsley aliyejifunga, wakati mabao ya wenyeji yalifungwa na Altidore na Bardsley.
Fulham walitangulia kupata bao kupitia kwa Dejagah kipindi cha pili, lakini Chiriches akaisawazishia Tottenham Hotspur na Holtby akaifungia la ushindi.
Everton wakishangilia jana
Mana City wakishangilia jana
![]() |
| Chelsea wakishangilia jana |
Baada ya matokeo ya mechi za jana usiku, Arsenal inaendelea kuongoa Ligi Kuu England kwa pointi zake 34 ilizovuna kwenye mechi 14, Chelsea ya pili kwa pointi zake 30 mechi 14 pia, Man City ya tatu pointi 28 mechi 14 pia, Liverpool ya nne pointi 27 mechi 14 pia Everton ya tano pointi 27 mechi 14 pia na Spurs ya sita pointi 24 mechi pia, wakati mabingwa watetezi, United wenye pointi 22 wapo nafasi ya tisa.

.png)
0 comments:
Post a Comment