• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 14, 2013

  BAYERN YAMALIZA MWAKA BILA KUFUNGWA HATA MECHI MOJA BUNDESLIGA

  MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich wameendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika mechi 41 za Ligi ya Ujerumani, Bundesliga kufuatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Hamburg SV leo.
  Bayern, ambayo haitashuka dimbani wiki ijayo, wamemaliza mwaka mzima bila kufungwa, huku mechi yao ya mwisho kufungwa Bundesliga ilikuwa ni Oktoba 2012.

  Huku Franck Ribery na David Alaba wakiwa benchi na Arjen Robben majeruhi, Bayern walisotea ushindi mbele ya Hamburg, ambayo msimu uliopita waliifunga kiulaini mabao 9-2.
  Mario Mandzukic alifunga la kwanza dakika ya 42, Mario Goetze akafunga la pili dakika ya saba kipindi cha pili, kabla ya Xherdan Shaqiri kumaliza kazi dakika ya mwisho.
  Hamburg ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 87 kupitia kwa Pierre-Michel Lasogga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BAYERN YAMALIZA MWAKA BILA KUFUNGWA HATA MECHI MOJA BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top