• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 21, 2013

  ASHANTI YAONGOZA KUSAJILI DIRISHA DOGO, YAKUSANYA MAKINDA NA 'WALIOSHINDIKANA'

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura amesema kwamba Desemba 23 mwaka huu ndiyo mwisho wa kipindi cha pingamizi kwa usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
  Wambura amesema katika VPL, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Coastal Union ndiyo timu pekee kati ya 14 za ligi hiyo ambazo hazikuwasilisha maombi ya usajili katika dirisha dogo.
  Ashanti imeongoza kusajili wapya dirisha dogo

  Amesema Ashanti United ndiyo inayoongoza kwa wachezaji 15 ambao ni Kassim Kilungo, Mohamed Banka, Bright Obinna, Victor Costa, Juma Mpongo, Juma Jabu, Ally Kondo, Shafii Rajab, Mohamed Faki, Abubakar Mtiro, Patrick Mhagama, Ally Kabunda, Hassan Kabunda, Idd Ally na Rahim Abdallah.
  Ruvu Shooting; Ally Khan na Jumanne Khamis, Rhino Rangers; David Siame, John Kauzeni, Salum Mamlo, Jingo Seleman, Darlington Enyinna, Rajab Twaha, Godfrey Mobi na Mussa Digubike. Mbeya City; Saad Kipanga. Tanzania Prisons; Dennis Liwanda, Godfrey Pastory, Henry Mwalugala, Jamal Salum na Brayton Mponzi.
  Oljoro JKT; Jacob Masawe, Mansour Ali, Juma Mohamed, Amour Mohamed, Mohamed Ali, Mussa Nahoda, Benedict Ngasa, Seleman Makame, Shija Mkina, Ali Omar na Shaweji Yusuf. Simba; Uhuru Selemani, Ivo Mapunda, Ali Badru, Awadh Juma, Donald Mosoti na Yaw Berko. Azam; Mouhamed Kone.
  Yanga; Hassan Dilunga, Juma Kaseja na Emmanuel Okwi. Mgambo Shooting; Suleiman Khatib, Bolly Ajali, Amri Sambinga na Issa Ali. JKT Ruvu; Chacha Marwa, Sino Augustino, Idd Mbaga na Cecil Luambano.
  Wakati huo huo: Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itakutana Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jamal Malinzi katika kikao kitakachofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kupitia ajenda mbalimbali ikiwemo uundwaji wa vyombo vya haki (Kamati ya Nidhamu, Kamati ya Maadili na Kamati ya Uchaguzi).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ASHANTI YAONGOZA KUSAJILI DIRISHA DOGO, YAKUSANYA MAKINDA NA 'WALIOSHINDIKANA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top