• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 20, 2013

  MESSI AUWASHA MOTO BARCELONA, AMUAMBIA MKURUGENZI HAJUI LOLOTE KUHUSU SOKA

  MSHAMBULIAJI Lionel Messi amewasha moto Barcelona baada ya kumuambia Mkurugenzi wake hajui lolote kuhusu soka.
  Maelezo hayo ni majibu kwa Javier Faus ambaye wiki mbili zilizopita alisema kwamba Barcelona haina sababu ya kuketi chini na mwanasoka huyo kujadili Mkataba wake wa sasa. 
  Amejibu: Lionel Messi amesema Mkurugenzi wa Barcelona, Javier Faus hajui lolote kuhusu soka baada ya kusema hakuna haja ya kujadili Mkataba wa sasa wa Muargentina huyo
  Lionel Messi
  Akizungumza na Redio ya Catalan, RAC1 kutoka Argentina, Messi alisema: "Barcelona ni klabu bora duniani, inawakilishwa na wajumbe bora wa bodi pia. Senor [Javier] Faus ni mtu ambaye hajui lolote kuhusu soka na anataka kuongoza Barcelona kama biashara, ambayo siyo,".
  Alisema: "Mbali na hayo, ningemkumbusha kwamba hata hakuna mtu yeyote kutoka kambi yangu ameulizia kuhusu ongezeko lolote la mshahara na anafahamu hilo,".
  Golden boy: Messi is Barca's prize asset and won the European Golden Boot for 2013
  Mwana wa dhahabu: Messi ni bidhaa adimu ndani ya Barca na ndiye mahinsi wa Kiatu cha Dhahabu Ulaya mwaka 2013
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AUWASHA MOTO BARCELONA, AMUAMBIA MKURUGENZI HAJUI LOLOTE KUHUSU SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top