• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 16, 2013

  AZAM TV YAANZA RASMI MAUZO NA HUDUMA OFISI KUU TAZARA

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  KAMPUNI ya AzamTV leo imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
  Huduma za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6, 2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi kungalia bure hadi hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa mwezi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Limited, Yussuf Bakhresa kushoto akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi kuu ya huduma kwa wateja ya Azam TV, zilizopo makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la TAZARA mjini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington.

   Kwa kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo ni:

  Azam One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.
  Azam Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia  
  SinemaZetu – Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
  Kwa pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya michezo, tamthilia, watoto na maisha.
  Ofisi ilifunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd.
  “Ofisi hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha nia thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika. Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema Bakhresa
  Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV  ipo sokoni kwa ajili ya kila mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote nchini. Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – situ katika ofisi hizi lakini pia kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa. AzamTV ni ya kudumu”
  Azam Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa Tanzania.
  Wateja wakisubiri kuhudumiwa
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tabasamu PR, Lucy Ngongoseke kushoto akimuelekeza jambo Yussuf Bakhresa
  Yussuf akifunua keki za Azam TV

  Yussuf akizungumza na wasanii
  Yussuf anakula keki
  Keki ya Azam TV

  Maofisa wa Azam Media wakitoa huduma
  Mteja akihudumiwa
  Yussuf akisaini autograph 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM TV YAANZA RASMI MAUZO NA HUDUMA OFISI KUU TAZARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top