• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 14, 2013

  ARSENAL MBIONI KUSAJILI KIFAA CHA BARCA, KILA KITU TAYARI BAADA YA KUMALIZANA TU

  WINGA wa Barcelona, Toni Sanabria anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka mitano na Arsenal baada ya kuwaambia vigogo hao wa Hispania anataka kuondoka.
  Sanabria, mwenye umri wa miaka 17, anataka kufuata nyayo za wachezaji kadhaa makinda wa Barca, wakiwemo Cesc Fabregas, Fran Merida, Hector Bellerin na Jon Toral kuhamia London Kaskazini kutoka Katalunya.
  Mshambuliaji huyo wa Paraguaya ameivutia klabu ya Roma, lakini Arsenal iko tayari kuipiga bao klabu hiyo ya Italia kwa kumpa kinda huyo Mkataba mnono zaidi.
  Anaondoka: Kinda wa Barca, Toni Sanabria (kushoto) yupo karibu kujiunga na Arsenal baada ya kuiambia klabu yake ya Hispania anataka kuondokaDeal: Sanabria's representatives are due in London next week with Arsenal expected to pay around £300k in compensation
  Dili: Wawakilishi wa Sanabria wanatarajiwa kufika London wiki ijayo kwa mazungumzo na Arsenal, inayotarajiwa kutoa Pauni 300,0000.
  Wakala wake, Raul Verdu amesema: "Mkataba wetu na Arsenal ni mzuri zaidi na tunatarajia kufikia mwafaka wiki ijayo,". Arsenal inatarajiwa kukutana na Barcelona na Sanabria wiki ijayo kumaliza suala hilo pamoja na mamlaka za soka zitoe baraka zake.
  The Gunners wanatarajiwa kutoa jumla ya kiasi cha Pauni 300,000 kwa ajili ya Sanabria.
  Talented teen: Sanabria is the youngest player to ever be capped by the Paraguay national side
  Sanabria ni kinda mwenye kipaji ambaye ameweka rekodi ya mchezaji mdogo zaidi kuchezea timu ya taifa ya ParaguayEarly move: Cesc Fabregas moved from Barcelona to Arsenal as a teenager but eventually returned to the club of his youth
  Alifungua njia: Cesc Fabregas alihamia Arsenal kutoka Barcelona akiwa kinda, lakini akarejea klabu yake akiwa kijana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL MBIONI KUSAJILI KIFAA CHA BARCA, KILA KITU TAYARI BAADA YA KUMALIZANA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top