• HABARI MPYA

    Thursday, March 01, 2012

    HISPANIA YAUA 5-0 BILA TORRES, VILLA, MAREKANI YAIDUWAZA ITALIA NYUMBANI


    ZIKIWA zimebaki siku 100 kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Italia imefungwa na Marekani kwa mara ya kwanza ndani ya mechi 11 zaidi ya miaka 78, wakati Hispania, Ufaransa na Uholanzi wanaendelea vizuri baada ya kupata ushindi mnono.
    Clint Dempsey alipiga bao katika dakika ya 55 Genoa na Wamarekani wakaibuka na ushindi wa 1-0 Jumatano usiku.
    Roberto Soldado alipiga mabao matatu peke yake wakati mabingwa wa Ulaya, Hispania wanashinda 5-0 dhidi ya Venezuela mjini Malaga. Ufaransa iliendeleza rekodi yake ya kutofungwa katika mechi 18 wakati Oliver Giroud na Florent Malouda walitupia nyavuni katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Ujerumani mjini Bremen.
    Uholanzi ilishinda 3-2 dhidi ya England wakati Arjen Robben akifunga bao lake la pili dakika ya mwisho. Hicho ni kipigo cha kwanza kwa kocha Stuart Pearce katika mechi ya kwanza akiwa kazini.
    Lionel Messi alifunga hat trick hyake ya kwanza na kuiwezesha Argentina kuifunga Uswisi 3-1.
    Saudi Arabia ilitolewa katioka mechi za kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 kwa kufungwa mabao 4-2 na Australia, wakati Korea Kusini, Lebanon, Oman na Qatar zimetinga raundi ya mwisho ya mchujo.
    Katika mchezo mwingine baadaye sana, Colombia iliifunga Mexico 2-0 mjini Miami na Chile ilitoka sare ya 1-1 na Ghana mjini Chester, Pa.
    Estonia iliifunga El Salvador 2-0 mjini Los Angeles katika mchezo ambao refa aliumaliza baada ya dakika 89 baada ya mashabiki kuwatupia vitu marefa wenzake.
    Makocha wengi Ulaya wako chini ya jakamoyo kuelekea fainali za Ulaya zinazoandaliwa kwa pamoja na Poland na Ukraine, ambazo zitaanza Juni 8.
    Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew akiwa miongoni mwao, anafanya kazai kubwa ya kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia kuelekea michuano hiyo.
    Lakini Ufaransa inaweza kuwa na matumaini japo bila ya wachezaji wake kadhaa tegemeo kutokana na ushindi wao.
    Les Bleus walionyesha soka ya nguvu katika mechi hiyo na Giroud, anayeongoza kwa mabao kwenyen ligi ya Ufaransa, aliwafungia wageni bao la kuongoza dakiika ya 21.
    Malouda alipiga la pili dakika ya 69 kabla ya Cacau kuifungia Ujerumani la kufutia machozi dakika za majeruhi.
    Ufaransa ambayo ililazimika kucheza mechi maalum ya kuwania kiufuzu Euro ya mwaka huu, haijafungwa tangu ifungwe 1-0 na Belarus Septemba 3, 2010.
    Ikicheza bila ya mfungaji wake bora, David Villa ambaye ni majeruhi na mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres aliyetwam kikosini Hispania kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano, mshambuliaji wa Valencia, Soldado alichezea kwa mara ya kwanza timu ya taifa ndani ya miaka mine na kufunga mabao matatu, kabla kocha Vicente del Bosque kuchagua kikosi chake cha kwenda nacho kutetea Kombe.
    Cesc Fabregas aliwatengenezea mabao Andres Iniesta na David Silva kabla ya mapumziko na Soldado akapiga matatu. Hispania imeshinda mechi zake zote nne dhidi ya Venezuela.
    England ilionekana kukaribia kupata sare dhidi ya Uholanzi kwa Gary Cahill kufunga dakika ya 85 na Ashley Young dakika ya 90, lakini Arjen Robben alifunga bao lake la pili dakika ya mwisho  na kuzima ndoto za sare kwa Three Lions.
    Ireland ilipata sare ya 1-1 na Jamhuri ya Czech Republic, ambao pia wamefuzu, wakati Simon Cox alipofunga zikiwa zimesali9a dakika nne. Milan Baros aliwafungia bao la kuongoza Czech dakika ya 50.
    Poland na Ureno zilitoka 0-0 katika mechyi ya kwanza kuchezwa kwenye Uwanja wa taifa, mchezo utakaobeba mechi ya ufunguzi ya Euro. Ukraine ilishinda 3-2 dhidi ya Israel.
    Sweden ilishinda 3-1 dhidi ya Croatia, Ugiriki ilitoka 1-1 na Ubelgiji na Urusi ilishinda 2-0 dhidi ya Denmark.
    Wales ilifungwa 1-0 na Costa Rica mjini Cardiff, mchezo ambao wenyeji walikuwa na matumaini ya kushinda kumuenzi aliyekuwa kocha wao, Gary Speed.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HISPANIA YAUA 5-0 BILA TORRES, VILLA, MAREKANI YAIDUWAZA ITALIA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top