• HABARI MPYA

  Friday, March 08, 2019

  SERENGETI BOYS YAPATA KIPIGO KINGINE, YACHAPWA 5-0 NA UTURUKI MICHUANO YA UEFA ASSIST

  Na Mwandishi Wetu, ANTALYA
  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imekamilisha mechi zake za Kundi A michuano ya UEFA Assist kwa kuchapwa mabao 5-0 na wenyeji, Uturuki katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Emirhan Sports Complex mjini Antalya.
  Mabao ya Uturuki yalifungwa na Nuri Emre Aksit dakika ya 43, Muhammed Akpinar dakika ya 44, Ali Akman dakika ya 52, Salih Kavrazil dakika ya 84 na Karakaya dakika ya 89.
  Matokeo hayo yanafuatia Serengeti Boys kufungwa 1-0 na Guinea kabla ya kuifunga 3-2 Australia katike mechi zake mbili zilizotangulia za kundi hilo. 
  Mchezaji wa Serengeti Boys, Edson Mshirakandi akimmtoka mchezaji wa Uturuki leo mjini Antalya

  Wakati Kundi A linaundwa na Tanzania, Guinea, Australia na wenyeji, Uturuki, Kundi B linazikutanisha Cameroon, Uganda, Morocco na Belarus na Kundi C lina timu za Senegal, Nigeria, Angola na Montenegro. 
  Tanzania ilitumia michuano hiyo kama maandalizi yake ya mwisho ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) ambayo wao watakuwa wenyeji kuanzia Aprili 14 hadi 28 mjini Dar es Salaam.
  Tanzania imepangwa Kundi A pamoja na Nigeria, Uganda na Angola wakati Kundi B linaundwa na timu za Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAPATA KIPIGO KINGINE, YACHAPWA 5-0 NA UTURUKI MICHUANO YA UEFA ASSIST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top