• HABARI MPYA

  Tuesday, March 05, 2019

  HIMID MAO ACHEZA MECHI YOTE TIMU YAKE YACHAPWA 4-0 NA AL AHLY LIGI YA MISRI

  Na Mwandishi Wetu, CAIRO
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami jana amecheza kwa dakika zote 90, timu yake, Petrojet FC ikichapwa mabao 4-0 na Al Ahly katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Petrosport mjini Cairo.
  Mabao ya Al Ahly yamefungwa na Junior Ajayi dakika ya nane akimalizia pasi ya Nasser Maher, Marwan Mohsen dakika ya 31 akimalizia pasi ya Geraldo aliyefunga la tatu dakika ya 69 kwa pasi ya Ali Maaloul na Karim Nedved aliyefunga la tano dakika ya 75.
  Nedved aliyefunga akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la pili la Al Ahly, Marwan Mohsen angeweza kufunga mabao zaidi kama angetumia vyema nafasi nyingine alizopata.
  Kwa ushindi huo, Al Ahly inafikisha pointi 51 baada ya kucheza mechi 22, ikipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Zamalek inayoongoza kwa pointi zake 52 za mechi 21.  Petrojet yenyewe inabaki nafasi ya 13 na pointi zake 25 za mechi 26 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Misri inayoshirikisha timu 18.
  Watanzania wengine wanaocheza ligi hiyo, kiungo Shiza Kichuya timu yake ENPPI inashika mkia kwa pointi zake 21 za mechi 24 na mshambuliaji Yahya Zayd, timu yake Ismailia inashika nafasi ya tisa kwa pointi zake 28 za mechi 20.   
  Kikosi cha Al Ahly kilikuwa; Mohamed El Shenawy, Yasser Ibrahim, Ayman Ashraf, Ali Maaloul/ Rami Rabia dk72, Mohamed Hany, Hamdi Fathi/ Hesham Mohamed dk45, Nasser Maher, Karim Nedved, Marwan Mohsen/ Walid Azarou dk76, Junior Ajayi na Geraldo.
  Petrojet; Mohamed Aboul-Naga, Ahmed Abdulrasol, Ibrahim Al-Qadi/Hossam Hassan dk78, Hamada Tolba, Ahmed Afifi, Ahmed Safy, Ahmed El Agouz, Himid Mao, Ahmed Abdelrahman Zola, Vieira Sanogo/Ahmed Temsah dk43 na Chris Gadi/Mahmoud Emad dk85. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIMID MAO ACHEZA MECHI YOTE TIMU YAKE YACHAPWA 4-0 NA AL AHLY LIGI YA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top