• HABARI MPYA

  Thursday, October 04, 2018

  ENYIMBA YAPIGWA 1-0 NA RAJA CASABLANCA KOMBE LA SHIRIKISO

  Na Mwandishi Wetu, ABA
  BAO pekee la mshambuliaji Abdelilah Hafidi limeipa ushindi wa ugenini wa 1-0 Raja Casablanca dhidi ya wenyeji, Enyimba International katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika usiku wa Jumatano Uwanja wa Enyimba International mjini Aba, Nigeria.
  Hafidi alifunga bao hilo dakika ya 48 akimalizia pasi ya kiungo  Mmorocco mwenzake, Zakaria Hadraf kumtungua kipa Joel Theophil Afelokhai.
  Sasa Raja watakuwa na kazi nyepesi ya kuulinda ushindi wao mwembamba katika mchezo wa marudiano Oktoba 24 mjini Casablanca nchini Morocco ili waingie fainali ya michuano hiyo namba mbili kwa ukubwa barani.

  Katika mchezo mwingine wa Nusu Fainali ya kwanza usiku wa Jumatano Uwanja wa Al Masry Club mjini  Port Said, wenyeji Al Masry wamelazimishwa sare ya bila kufungana na  AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ENYIMBA YAPIGWA 1-0 NA RAJA CASABLANCA KOMBE LA SHIRIKISO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top