• HABARI MPYA

    Monday, October 08, 2018

    COASTAL UNION YAWEKWA CHINI YA UANGALIZI KWA VURUGU ZA MASHABIKI, WAKIRUDIA MKWAKWANI UNAFUNGIWA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeamua timu ya Coastal Union ya itakuwa kwenye uangalizi kwa mechi mbili zijazo za Uwanja wa nuyumbani, Mkwakwani mjini Tanga kufuatia tuhuma za mashabiki wake kuvamia uwanjani. 
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 
    Mashabiki wa wanadaiwa kuingia uwanjani baada ya mechi namba 24 dhidi ya KMC FC iliyomalizika kwa sare ya 0-0 Septemba 1, 2018 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, huku waamuzi na wachezaji wakiwa bado hawajatoka, kitendo ambacho ni hatari kiusalama.
    “Kamati imeamua kuwa Coastal Union itakuwa kwenye kipindi cha uangalizi kwa mechi mbili zijazo, na iwapo washabiki wataendelea kuingia ndani ya uzio, timu hiyo itafungiwa kuutumia uwanja huo,” amesema Wambura.
    Aidha, Wambura amesema kwamba Ruvu Shooting imepewa onyo kali kwa kutowasilisha orodha ya wachezaji wake katika kikao cha maandalizi ya mechi namba 34 dhidi ya Tanzania Prisons iliyomalizika kwa sare ya 2-2 Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
    Mwamuzi Msaidizi wa mechi namba 41 kati ya Lipuli FC walioshinda 1-0 dhidi ya Alliance FC ya Mwanza, Idd Mikongoti wa Dar es Salaam amefungiwa miezi sita kwa kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea, hivyo kukataa bao lililofungwa na Alliance FC Septemba 19, 2018 Uwanja wa Samora mjini Iringa. 
    Wambura amesema kwamba adhabu ya refa huyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YAWEKWA CHINI YA UANGALIZI KWA VURUGU ZA MASHABIKI, WAKIRUDIA MKWAKWANI UNAFUNGIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top