• HABARI MPYA

    Monday, October 08, 2018

    BOCCO AFUNGIWA MECHI TATU NA KUPIGWA FAINI YA SH. 500,000 KWA KUMCHAPA KONDE MCHEZAJI WA MWADUI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga ngumi mcheza wa Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Septemba 23, 2018 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 
    John Bocco amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga ngumi mcheza wa Mwadui FC

    Wambura amesema kwamba baada ya Bocco kutolewa kwa kadi nyekundu katika mechi hiyo namba 52, Simba SC ikishinda 3-1 yeye akifunga mabao mawili, adhabu nyingine ni kukosa mechi tatu na faini ya Sh. 500,000.
    Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji na tayari Bocco amekwishakosa mechi mbili dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga Septemba 30 na dhidi ya African Lyon Jumamosi zote Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BOCCO AFUNGIWA MECHI TATU NA KUPIGWA FAINI YA SH. 500,000 KWA KUMCHAPA KONDE MCHEZAJI WA MWADUI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top