• HABARI MPYA

  Friday, October 20, 2017

  MBEYA CITY YAWEKA MALENGO YA KUSHINDA MECHI ZOTE NYUMBANI NA HAKUNA KUFUNGWA UGENINI

  Na David Nyika, MBEYA
  TIMU ya Mbeya City FC imesema itapambana kuanzia sasa kuhakikisha inashinda mechi zote zilizobaki za nyumbani za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Pamoja na hayo, Mbeya City, maarufu kama timu ya Kizazi Kipya mjini hapa imesema pia haitaki kupoteza mechi yoyote ugenini tena kwa kuhakikisha kama si kushinda basi wanatoa sare.
  Hayo yamesemwa na Meneja wa Mbeya City FC, Geoffrey Katepa katika mahojiano na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Mbeya kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting.
  “Baada ya kupata sare Mwanza na Mbao FC (2-2), tunataka tuendeleze rekodi ya kutofungwa katika mechi zetu zote. Za nyumbani lazima tupigane tushinde, za ugenini hata tukitoa sare si vibaya, lakini lengo ni kushinda mechi zote ili tumalize katika nafasi nzuri,”amesema Katepa.  
  Kocha Mrundi Nswanzurino Ramadhani (kulia) akiwangoza wachezaji wa Mbeya City mazoezini 

  Kiungo huyo wa zamani wa Yanga, amesema kwamba katika mchezo wa kesho na Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya watahakikisha wanashinda ili kutimiza azma yao.
  Amesema walianza vibaya Ligi Kuu kwa sababu ya kuchelewa kuanza maandalizi ya msimu mpya, lakini baada ya hapo wakajiimarisha na sasa timu yao iko vizuri.
  Amesema na ujio wa kocha mpya, Mrundi Nswanzurino Ramadhani ndiyo umekuja kuiimarisha timu zaidi, hivyo ni matarajio yao makali ya Mbeya City yatarudi. 
  Mbeya City kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake nane baada ya kucheza mechi sita, ikishinda mbili, sare mbili na kufungwa mbili, moja nyumbani dhidi ya Ndanda FC 1-0.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAWEKA MALENGO YA KUSHINDA MECHI ZOTE NYUMBANI NA HAKUNA KUFUNGWA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top