• HABARI MPYA

    Monday, September 11, 2017

    TIMU YA POLISI TANZANIA YAPATIWA MSAADA WA JEZI NA FEDHA

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya SportPesa imetoa vifaa vya michezo pamoja na fedha taslimu Sh. Milioni 20 kwa timu ya soka ya Polisi Tanzania.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo wakati wa mabakidhiano hayo kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema kwamba wanatambua mchango wa jeshi la Polisi kwa jamii, kwani linafanya kazi kubwa kuhakikisha nchi na wananchi wanakuwa salama.
    Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas akimkabidhi jezi IGP, Simon Sirro leo mjini Dar es Salaam

    Akizungumza kwa niaba ya timu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro  amesema kwamba wanashukuru kwa mchango wao kwa sababu ni moja ya kuleta maendeleo katika timu hiyo.
    “Tunatanguliza shukrani za dhati kwa SportPesa kwa vifaa hivi pamoja na fedha hizi na tuna waahidi hatutawaangusha, kwani timu yetu ilikuwa na uhaba wa vifaa mbalimbali na fedha mlizotupatia zitaisaidia timu kutatua shida mbalimbali,” amesema Sirro.
    SportPesa ni kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ambayo pia inazidhamini klabu tatu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba, Yanga na Singida United tangu ilipoanza rasmi uendeshaji wa shughuli zake za kibiashara nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU YA POLISI TANZANIA YAPATIWA MSAADA WA JEZI NA FEDHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top