• HABARI MPYA

    Friday, April 08, 2016

    YANGA NA AL AHLY LIVE KESHO AZAM TV

    YANGA imeiuzia Azam TV haki za kurusha mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Maana yake kesho Watanzania wote wataushuhudia mchezo huo kupitia Televisheni nchini.
    Azam TV wamefanikiwa kupata haki hizo baada ya kuwapiku Al Ahly ambao pia walikuwa wanataka haki za kurusha mechi hiyo.
    Mapema jana Yanga iliwagoma Al Ahly kurusha matangazo ya mechi hiyo.
    Yanga watakuwa wenyeji wa Ahly kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika na Ahly walitaka wachukue matangazo kwa ajili ya kurusha Misri tu.
    Hata hivyo, leo uongozi wa Ahly umethibitisha rasmi kwamba umenyimwa haki hiyo na utaonyesha mechi hiyo kupitia mitandao tu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA AL AHLY LIVE KESHO AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top