• HABARI MPYA

  Sunday, April 02, 2023

  YANGA SC YAWAPIGA TP MAZEMBE 1-0 NA PALE PALE LUBUMBASHI


  BAO pekee la Farid Mussa dakika ya 63 limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, TP Mazembe katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Yanga SC inamaliza na pointi 13, ikiendelea kuongoza mbele ya Monastir ya Tunisia yenye pointi 10 ambayo baadaye usiku itamenyana na Real Bamako Jijini Tunis.
  Kama Monastir watashinda kwa wastani wa zaidi ya mabao matatu basi wataongoza kundi hilo dhidi ya wana Robo Fainali wenzao, Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAWAPIGA TP MAZEMBE 1-0 NA PALE PALE LUBUMBASHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top