• HABARI MPYA

    Tuesday, February 17, 2026

    SIMBA SC YATINGA RAUNDI YA TATU KOMBE LA CRDB

    VIGOGO, Simba SC wamefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Greenland ya Kagera usiku huu Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC yamefumgwa na Baraka Mwangosi dakika ya 13, beki Anthony Mligo dakika ya 45’+3 na kiungo wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Neo Maema dakika ya 90.
    Mechi nyingine ya leo Kombela CRDB wenyeji, KMC FC wameaga mashindano baada ya kuchapwa 3-2 na Bandari Tanzania jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Jumla ya timu 64 zinashiriki hatua hii na kesho mabingwa watetezi, Yanga wataanza kampeni yao ya kutetea taji lao hilo kwa mwaka wa tano mfululizo watakapomenyana na mabingwa wa kwanza wa Ligi Kuu ya nchi, Cosmopolitan ya Dar es Salaam pia. 

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA RAUNDI YA TATU KOMBE LA CRDB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top