• HABARI MPYA

  Sunday, April 02, 2023

  GOMEZ APIGA MBILI SINGIDA YAICHAPA MBEYA CITY 4-1


  TIMU ya Singida Big Stars imekuwa ya kwanza kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Mbeya City leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na Mbrazil, Bruno Gomes mawili dakika ya saba na 57, Mghana Bright Adjei dakika ya 10 na Mkongo Fancy Kazadi dakika ya 17, wakati la Mbeya City limefungwa na mtokea benchi Eliud Ambokile dakika ya 55.
  Kwa matokeo hayo, Singida Big Stars itakutana na mshindi kati ya Yanga na Geita Gold katika Nusu Fainali mwishoni mwa mwezi huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOMEZ APIGA MBILI SINGIDA YAICHAPA MBEYA CITY 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top