• HABARI MPYA

  Saturday, April 01, 2023

  PAMBA YAAMBULIA SULUHU KWA KITAYOSCE NYAMAGANA


  WENYEJI, Pamba leo wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Kitayosce katika mchezo wa Ligi ya Championship kuwania kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Mechi nyingine za Championship leo, vinara JKT Tanzania wamewatandika Mbuni FC 4-0, Mbeya Kwanza imetoka sare ya 1-1 na Green Warriors na Fountain Gate imeichapa 2-0 African Sports.
  Msimamo wa Championship sasa JKT Tanzania ina pointi 59 kileleni, ikifuatiwa na Kitayosce pointi 50 baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Pamba ni ya tatu kwa pointi zake 48 za mechi 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMBA YAAMBULIA SULUHU KWA KITAYOSCE NYAMAGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top