• HABARI MPYA

  Saturday, April 01, 2023

  ARSENAL YAWACHAPA LEEDS UNITED 4-1 EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Jesus mawili, kwa penalti dakika ya 35 na 55 akimalizia pasi ya Leandro Trossard, mengine Benjamin White dakika ya 47 na Granit Xhaka dakika ya 84, wakati la Leeds United limefungwa na Rasmus Kristensen dakika ya 76.
  Ushindi huo unaifanya Arsenal ifikishe pointi 72 katika mchezo wa 29 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi, wakati Leeds United inabaki na pointi zake 26 za mechi 28 nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAWACHAPA LEEDS UNITED 4-1 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top