• HABARI MPYA

  Saturday, April 01, 2023

  NGOLO KANTE ATOKEA BENCHI CHELSEA YACHAPWA 2-0


  KIUNGO Mfaransa, N'Golo Kante ametokea benchi leo timu yake, Chelsea ikichapwa 2-0 na Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  N'Golo Kante aliingia dakika ya 57 kuchukua nafasi ya Muingereza, Ruben Ira Loftus-Cheek kwenda kucheza kwa mara ya kwanza chini ya kocha Graham Potter na kwa mara ya kwanza tangu Agosti.
  Aliingia wakati Aston Villa tayari wamekwishapata mabao yao yaliyofungwa na Ollie Watkins dakika ya 18 na John McGinn dakika ya 56.
  Kwa matokeo hayo, Aston Villa inafikisha pointi 41 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 38 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGOLO KANTE ATOKEA BENCHI CHELSEA YACHAPWA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top