• HABARI MPYA

  Sunday, April 02, 2023

  JOSHUA AMSHINDA MMAREKANI KWA POINTI, AMTAKA FURY


  BONDIA Muingereza, Anthony Joshua (kulia) usiku wa Jana amefanikiwa kumshinda kwa pointi Mmarekani, Jermaine Franklin katika pambano la uzito wa juu ngumi za kulipwa ukumbi wa O2 Arena, Greenwich kuzipiga.
  Pamoja na ushindi huo, lakini hakuwa AJ yule ambaye walimzoea kumuona kwa ubora wa hali ya juu ulingoni kabla ya kupoteza mapambano mawili mfululizo mbele ya Olexsandr Usyk wa Ukraine na kuvuliwa mataji yake ya IBF, IBO, WBA na WBO.
  Baada ya pambano hilo Anthony Joshua alisema anamtaka Muingereza mwenzake na bingwa wa WBC, Tyson Fury.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA AMSHINDA MMAREKANI KWA POINTI, AMTAKA FURY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top