• HABARI MPYA

  Saturday, April 01, 2023

  MAN CITY YAIBAMIZA LIVERPOOL 4-1 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City wameitandika Liverpool mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Julian Alvarez dakika ya 27, Kevin De Bruyne dakika ya 46, Ilkay Gundogan dakika ya 53 na Jack Grealish dakika ya 74, wakati la Liverpool limefungwa na Mohamed Salah dakika ya 17.
  Manchester City inafikisha pointi 64 katika mchezo wa 28, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nane na Arsenal ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Liverpool inabaki na pointi 42 za mechi 27 nafasi ya nane.
  Kwa upande wao Liverpool baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 42 za mechi 26 nafasi ya sita.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIBAMIZA LIVERPOOL 4-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top