• HABARI MPYA

  Saturday, April 01, 2023

  JOSHUA KUZIPIGA NA MMAREKANI LEO 02 ARENA


  BONDIA Muingereza, Anthony Joshua (kushoto) leo anapanda ulingoni ukumbi wa O2 Arena, Greenwich kuzipiga na Mmarekani, Jermaine Franklin katika pambano la uzito wa juu ngumi za kulipwa.
  Joshua atakuwa anapigana kwa mara ya kwanza tangu apokonywe mataji yake ya IBF, IBO, WBA na WBO na Olexsandr Usyk wa Ukraine Agosti 20 mwaka jana ukumbi wa Jeddah Superdome, Jeddah, Saudi Arabia baada ya kupigwa kwa pointi.
  Lilikuwa pambano la pili mfululizo Joshua anapigwa na Usyk baada ya lile la Septemba 25, mwaka 2021 ukumbi wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA KUZIPIGA NA MMAREKANI LEO 02 ARENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top