• HABARI MPYA

    Sunday, May 24, 2026

    MTIBWA SUGAR YAAMBULIA SARE KWA JKT TANZANIA 2-2 JAMHURI


    TIMU ya Mtibwa Sugar imetoa sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
    Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na beki wa kati, Haroun Evody Lyawatwa dakika ya 35 na kiungo mshambuliaji, Fredrick Charles Magata kwa penalti dakika ya 68, wakati mabao yote ya JKT Tanzania yamefungwa na mshambuliaji Paul Peter Kasunda dakika ya 20 na 42.
    Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 27 ingawa inashuka kwa nafasi moja hadi ya 11, wakati JKT Tanzania inafikisha pointi 38 nayo inabaki nafasi ya tano baada ya timu hizo zote kucheza mechi 25 kwenye ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.   

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAAMBULIA SARE KWA JKT TANZANIA 2-2 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top