• HABARI MPYA

  Saturday, October 01, 2022

  LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE 3-3 NA BRIGHTON ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya 3-3 na Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino mawili dakika ya 33 na 54 na Adam Webster aliyejifunga dakika ya 63, wakati ya Brighton yote yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya nne, 17 na 83.
  Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 10 katika nafasi ya tisa, wakati Brighton imetimiza pointi 14 nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE 3-3 NA BRIGHTON ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top