• HABARI MPYA

  Saturday, October 01, 2022

  CHELSEA YAIBAMIZA CRYSTAL PALACE 2-1 LONDON


  TIMU ya Chelsea imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 38 na Conor Gallagher dakika ya 90, wakati la Crystal Palace limefungwa na Odsonne Edouard dakika ya saba.
  Kwa matokeo hayo, Chelsea imefikisha pointi 13 katika nafasi ya tano, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake sita nafasi ya 16 baada ya wote kucheza mechi saba. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAIBAMIZA CRYSTAL PALACE 2-1 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top