• HABARI MPYA

  Wednesday, September 08, 2021

  YANGA KUWAKOSA SITA DHIDI YA RIVERS

   VIGOGO Yanga SC watawakosa wachezaji wake sita katika mechi ya kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United Jumapili  Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kwa sababu mbili tofauti.
  Mabeki Yassin Mustapha na David Bryson na kiungo Mapinduzi Balama wote ni majeruhi na kwa pamoja hawapo kwenye programu ya kocha Mtunisia, Nasreddine Mabi.
  Aidha, beki Mkongo Djuma Shabani na mshambuliaji Fiston Mayele pamoja na kiungo Mganda, Khalid Aucho wote hawana leseni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na usajili wao kutokamilika kwa wakati.


  Watatu hao wamekwamishwa na Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kuchelewa kufika kwa wakati na kwa mujibu wa taratibu watakosa mechi zote za Hatua ya Awali ya michuano hiyo.
  Baada ya mchezo wa Jumamosi Dar es Salaam, Yanga itasafiri kwa ajili ya mechi marudiano Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.
  Kuelekea mchezo huo, Yanga imepata mechi tatu za kujipima nguvu, ikifungwa 2-1 na Zanaco ya Zambia Uwanja wa Benjamin Mkapa na kushinda 3-1 dhidi ya Friends Rangers na 1-0 dhidi ya Pan Africans Manzese kwenye kambi yake, Avic Town, Somangira, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUWAKOSA SITA DHIDI YA RIVERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top