• HABARI MPYA

  Monday, September 06, 2021

  GNABRI APIGA MBILI UJERUMANI YASHINDA 6-0

  UJERUMANI jana imeibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya Armenia katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia kwa Ulaya Uwanja wa Mercedes-Benz-Arena Jijini Stuttgart.
  Mabao ya Ujerumani yamefungwa na Serge Gnabry mawili dakika ya sita na 15, Marco Reus dakika ya 35, Timo Werner dakika ya 45, Jonas Hofmann dakika ya 52 na Karim Adeyemi dakika ya 90 na ushei.
  Sasa Ujerumani inafikisha pointi 12 na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi mbili zaidi ya Armenia, wakati, Romania ni ya tatu kwa pointi zake tisa ikifuatiwa na Macedonia Kaskazini pointi nane, Iceland pointi nne na Liechtenstein haina pointi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GNABRI APIGA MBILI UJERUMANI YASHINDA 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top