• HABARI MPYA

  Monday, September 06, 2021

  KINDA MSPANIOLA AWEKA REKODI US OPEN


  NAYE mvulana wa umri wa miaka 18, Carlos Alcaraz wa Hispania ameweka rekpodi ya ‘bwana mdogo’ zaidi kuwahi kutinga Robo Fainali ya U.S. Open tangu mwaka 1963 – kufuatia kumtoa Mjerumani Peter Gojowczyk (32) na sasa atamenyana na mchezaji bora namba 12 duniani, Felix Auger-Aliassime.
  Naye bingwa wa French Open, Barbora Krejcikova ametinga Robo Fainali ya michuano ya U.S. Open kwa ushindi wa seti 2-0 (6-3, 7-6) dhidi ya bingwa mara mbili wa michuano hiyo, Garbine Muguruza.
  Sasa binti huyo wa umri wa miaka 25 kutoka Jamhuri ya Czech atamenyana na mchezaji namba mbili duniani, Aryna Sabalenka kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KINDA MSPANIOLA AWEKA REKODI US OPEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top