• HABARI MPYA

  Monday, September 06, 2021

  LUKAKU AFUNGA KATIKA MECHI YA 100 UBELGIJI

  MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku jana amefunga bao la kwanza dakika ya nane akiichezea Ubelgiji kwa mara ya 100 ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Jamhuri Czech.
  Katika mchezo wa Kundi E kufuzu kombe la Dunia Uwanja wa Roi Baudouin Jijini Brussels, mabao mengine ya Ubelgiji yalifungwa na nyota wa Real Madrid, Eden Hazard dakika ya 41 na mtokea benchi Alexis Saelemaekers 56, tena akimalizia pasi ya Lukaku.
  Kwa matokeo hayo, Ubelgiji inafikisha pointi 13 na kuendelea kuongoza Kundi E kwa pointi sita zaidi ya Czech, wakifuatiwa na Wales yenye pointi sita, Belarus pointi tatu na Estonia ambayo haina pointi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AFUNGA KATIKA MECHI YA 100 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top