• HABARI MPYA

  Wednesday, September 08, 2021

  DEEPAY APIGA HAT TRICK UHOLANZI YASHINDA 6-1

  MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Memphis Depay jana amefunga mabao matatu Uholanzi ikiibuka ushindi wa 6-1 dhidi ya Uturuki katika mchezo wa Kundi G kufuzu Kombe la Dunia Uwanja wa Johan Cruijff Arena Jijini Amsterdam.
  Depay mchezaji wa zamani wa Manchester United ya England, alifunga mabao yake dakika za 16 akimalizia pasi ya Davy Klaassen, dakika 38 kwa penalti na 54. 
  Mabao mengine ya Uholanzi yalifungwa na Davy Klaassen dakika ya kwanza, Guus Til dakika ya 80 na Donyell Malen dakika ya 90, wakati la kufutia machozi la Uturuki lilifungwa na Cengiz Under. 


  Kwa ushindi huo, Uholanzi inafikisha pointi 13 baada ya mechi sita na kuendelea kuongoza Kundi G kwa wastani wa mabao tu dhidi ya Ureno yenye pointi 13 pia, wakati Uturuki ni ya tatu kwa pointi zake 11, ikifuatiwa na Montenegro pointi nane, Latvia pointi tano na Gibraltar inashika mkia haina pointi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DEEPAY APIGA HAT TRICK UHOLANZI YASHINDA 6-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top