TIMU ya Biashara United ya Mara imeondoka jana Jijini Dar es Salaam kwenda Djibouti kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, FC Dikhil.
Mechi hiyo inachezwa leo jioni Uwanja wa El Hadj Hassan Gouled Jijini Ville de Djibouti kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 18 hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment