• HABARI MPYA

  Friday, October 02, 2020

  ARSENAL YAITOA LIVERPOOL KWA MATUTA CARABAO, KUKUTANA NA MAN CITY

  Liverpool, ENGLAND

  ARSENAL imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Ligi England baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku wa jana Uwanja wa Anfield.

  Sasa The Gunners watakutana na Manchester City kwenye Robo Fainali ya michuano hiyo inayojulikana pia kama Carabao Cup mwezi Desemba. 

  Robo Fainali nyingine; Manchester United itamenyana na Everton, Tottenham Hotspur na Stoke City na Newcastle United na Brentford.

  Shujaa wa Arsenal jana alikuwa ni kipa wake, Bernd Leno aliyeokoa mikwaju ya penalti ya Harry Wilson na Divock Origi na waliofunga penalti za Liverpool ni James Milner, Georginio Wijnaldum, Takumi  Minamino na Curtis Jones.


  Bernd Leno alikuwa Shujaa wa Arsenal jana baada ya kuokoa penalti za Harry Wilson na Divock Origi wa Liverpool
   


  Mmisri Mohamed Elneny pekee alikosa upande wa Arsenal, wakati Alexandre Lacazette, Cédric Soares, Ainsley Maitland-Niles, Nicolas Pépé na Joe Willock wote walifunga.

  Liverpool: Adrian, Neco Williams, Rhys Williams, Van Dijk/Gomez dk61, Milner, Grujic, Jones, Wilson, Jota/Wijnaldum dk76, Minamino na Salah/Origi dk61.

  Arsenal: Leno, Cedric, Gabriel, Holding, Kolasinac, Willock, Xhaka, Pepe, Ceballos/Elneny dk68, Saka/Maitland-Niles dk86 na Nketiah/Lacazette dk82.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAITOA LIVERPOOL KWA MATUTA CARABAO, KUKUTANA NA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top