• HABARI MPYA

    Monday, July 06, 2015

    TIMU YA NGASSA YATWAA UBINGWA WA AFRIKA KUSINI

    Free State wakisherehekea ushindi wao wa SAB U21 ya Afrika Kusini
    TIMU ya Free State Stars ya Bethlehem, imetwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa miaka 21 Afrika Kusini, maarufu kama SAB U21Championship baada ya kuifunga Mpulamanga kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya 1-1.
    Michuano hiyo ya saba ya U21 inayoandaliwa na Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Afrika Kusini (SAB), ilifanyika Uwanja wa Giant mjini Soshanguve.
    Na Free State ambayo imemsajili Mrisho Ngassa wa Tanzania Mei mwaka huu kwa ajili ya kikosi cha kwanza, imeweka historia kwa kuwa timu ya kwanza kutetea taji hilo. Haukuwa ushindi mwepesi kwa Free State kwani walilazimika kuifunga timu ambayo imetoa mfungaji bora wa mashinfdano na mchezaji borsa, Siphamandla Dhlamini.
    Wasaka vipaji kadhaa walimiminika kwenye michuano hiyo ambayo imekuwa ikizalisha  nyota kibao wa taifa hilo kusaka vipaji vya kupandisha Ligi Kuu.

    SAFARI YA FREE STATE HADI UBINGWA SAB U21 2015 
    Mpumalanga
    1. Free State 2 – 1 Mpumalanga
    2. Mpumalanga 2 – 1 Western Cape
    3. Mpumalanga 4 - 1 Gauteng
    4. Mpumalanga 4 – 1 Northern Cape
    Free State
    1. Free State 2 – 1 Mpumalanga
    2. Gauteng 2 – 3 Free State
    3. Free State 2 – 3 Northern Cape
    4. Free State 3 – 0 Western Cape
    Nusu Fainali
    Mpumalanga 4 – 2 University Sport SA
    Limpopo 0 – 2 Free States
    Fainali:
    Mpumalanga (1) 1 – 1 (3) Free State

    WASHINDI WA TUZO ZA SAB U21
    Mwamuzi Bora Msaidizi: Bafana Magagula
    Refa Bora: Khotso Johanne
    Kocha Bora: Litheko Marago
    Mfungaji Bora: Siphamandla Dhlamini
    Kipa Bora: Kwanele Bidi
    Mchezaji Bora:  Siphamandla Dhlamini
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU YA NGASSA YATWAA UBINGWA WA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top