• HABARI MPYA

    Monday, July 06, 2015

    COASTAL UNION YAPATA UONGOZI MPYA, ‘CHIFU’ WAO NI DK. ALLY AHMED TWAHA

    Na Mwandishi Wetu, TANGA
    MWENYEKITI mpya wa Coastal Union ni Dk Ahmed Ally Twaha, kufuatia uchaguzi uliofanyika mjini Tanga akimuangusha aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo, Stephen Mnguto.
    Katika kura 205 zilizopigwa, Dk Twaha alipata 192, wakati mpinzani wake Steven Mnguto aliambulia kura 11, huku mbili zikiharibika.
    Salim Amir aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, alipata 193 za Ndiyo, tisa za Hapana nan ne ziliharibika. 

    Aidha, waliochaguliwa katika nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hassan Omary Bwana (kura 190), Hassan Ramadhan Muhsin (kura 190), Abdallah Zubeiry Ally (kura 188), Hussein Ally Mwinyi Hamis (kura 185), Aggrey Ally Mbapu (kura 179), Mohamed Rajabu (kura 179), Omary Hassan Mwambashi (kura 144) na Waziri Mohamed (kura 31).
    Kwa kuwa walikuwa wanatakiwa wajumbe saba tu kwa hiyo wajumbe walioshinda ni kuanzia moja mpaka saba.
    Kwa kawaida uchaguzi ulifanyika kwa utulivu ukiacha vurugu za hapa na palele wakati wa kuingia ukumbini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YAPATA UONGOZI MPYA, ‘CHIFU’ WAO NI DK. ALLY AHMED TWAHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top