• HABARI MPYA

    Friday, July 03, 2015

    KIIZA ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC NA KUSEMA; "UBINGWA LAZIMA MSIMU UJAO"

    Rais wa Simba SC, akibadilishana mikataba na Hamisi Kiiza leo
    MSHAMBULIAJI Hamisi Kizza amejiunga rasmi na Klabu ya Simba leo kwa kusaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufuzu vipimo vya afya leo mchana.
    Tovuti rasmi ya Simba SC imeandika leo kwamba Kiiza baada ya kusaini mkataba alisema; “Nimekuja na kitu tofauti kwa ajili ya wapenzi na wanachama wa Simba na wakae mkao wa kula maana ninaijua vizuri ligi ya Tanzania na kwa kushirikiana na wachezaji wenzang naamini tutafikia malengo ya kutwaa ubingwa msimu ujao wa ligi”.
    Hamis Kizza ni mchezaji kutoka Uganda ambaye pia anacheza timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIIZA ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC NA KUSEMA; "UBINGWA LAZIMA MSIMU UJAO" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top