• HABARI MPYA

    Friday, July 03, 2015

    CHELSEA YAFANYA KWELI, YAAMSAJILI FALCAO NA KUIPA MCHEZAJI MONACO

    KLABU ya Chelsea imemsajili Radamel Falcao kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Monaco, huku kinda wa Blues, Mario Pasalic akihamia kwa wapinzani kama sehemu ya makubaliano ya dili hilo.
    Mshambuliaji huyo wa Colombia atacheza Ligi Kuu ya England kwa msimu wa pili akiwa na kikosi cha Jose Mourinho, baada ya kushindwa kung'ara akiwa na Manchester United msimu uliopita.
    "Nina furaha sana kujiunga na Chelsea na nina hamu ya kuanza mazoezi na kusaidia dhamira yetu ya kutetea ubingwa na kupata mafaniko Ulaya," amesema Falcao.
    Chelsea goalkeeper Thibaut Courtois saves from Falcao last season; the two will now be reunited in London
    Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois akiokoa dhidi ya Radamel Falcao msimu uliopita; wawili hao sasa wanaungana London

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, aliitua Old Trafford msimu uliopita kama mmoja wa washambuliaji tishio Ulaya, lakini maumivu ya goti aliyoyapata wakati anacheza Monaco yalionekana kumpunguza makali.
    Kinda Mcroatia, Pasalic, ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Elche katika La Liga, sasa atakwenda kwa mkopo Monaco kama sehemu ya dili hilo.
    Falcao ataungana na Diego Costa, Thibaut Courtois na Filipe Luis, ambao wote wamewahi kuchezea Atletico Madrid, sambamba na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Colombia, Juan Cuadrado Uwanja wa Stamford Bridge. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YAFANYA KWELI, YAAMSAJILI FALCAO NA KUIPA MCHEZAJI MONACO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top