• HABARI MPYA

    Monday, June 08, 2015

    ADEBAYOR APOKEWA 'KIFALME' KIJIJINI KWAO, ASEMA; "MAISHA MAZURI"

    MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Emmanuel Adebayor aliye katika misukosuko ya kifamilia amepata mapokezi mazuri alipowasili kijijini kwao, Aneho nchini Togo katika jitihada za kutatua matatizo ya kifamilia yanayomkabili.
    Adebayor alipewa ruhusa kurejea nyumbani kwa ajili ya masuala hayo ya kifamilia na alikosa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya England. 
    Katika taarifa zake mfululizo alizokuwa akiposti kwenye mitando ya kijamii, Adebayor amekuwa akifafanua matatizo yake ya kifamilia na ilifika wakati akasema ameamua kuangalia maisha yake tu.
    Lakini licha ya matatizo yake hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa mwenye furaha wakati anakanyaga ardhi ya kwao, Aneho na kulakiwa na umari wa wanakijiji.
    Akiwa amevalia suti ya kimichezo na fulana kwa ndani yenye maandishi yenye kuelezea mapenzi yake kwa Togo, alikuwa mwenye tabasamu wakati akiwapungia mkono wanakijiji waliojitokeza kumlaki akiwasili.
    Na akaposti picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram, sambamba na maelezo; "Inaeleza jinsi gani ni baraka kiasi gani kurejea nyumbani na kuwatembelea watu (wako). 
    Maelezo kamili ya picha yalikuwa yanasema; "SEA (Sheyi Emmanuel Adebayor), siwezi kuelezea hisia nilizonazo kila wakati ninapokwenda nyumbani na kuwatembelea watu wangu. Ilikuwa ni baraka kukutana na watu wa Aneho siku nyingine,".
    Alionekana mwenye kujali wakati amebeba kikapu cha vyakula huku umati wa wanakijiji umemzunguka. Ilionekana amesahau kwa muda matatizo yake ya kifamilia na maelezo mengine ya picha yakisema; "Maisha ni mazuri,"
    Katika picha ya pili, ameposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiwa ameketi kwenye sofa ameshika bomba la shisha, na ameandika maelezo yanayosomeka; 'SEA (Sheyi Emmanuel Adebayor), wakati wa kupumzika na familia!!' akitumia tena hashtag ya 'Maidha Mazuri'.
    Licha ya kujaribu kutatua matatizo yake ya kifamilia, mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal amejizulia 'janga' lingine. Kocha wa timu ya taifa ya Togo, Tom Saintfiet amembwatukia Adebayor, kwa kushindwa kujiunga na kikosi kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika wikiendi hii.
    The striker was blasted by new Togo coach Tom Saintfiet after failing to turn up to international duty on time
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ADEBAYOR APOKEWA 'KIFALME' KIJIJINI KWAO, ASEMA; "MAISHA MAZURI" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top